Supervised user import: Listen for profile creation/deletion
[chromium-blink-merge.git] / chrome / app / resources / terms / terms_sw.html
blobedfc6ff08c3c3dbf485d8d2cc5dc1c7186f0d485
1 <!DOCTYPE HTML PUBLIC "-//W3C//DTD HTML 4.01 Transitional//EN"
2 "http://www.w3.org/TR/html4/loose.dtd">
3 <html DIR="LTR">
4 <head>
5 <meta http-equiv="Content-Type" content="text/html; charset=UTF-8">
6 <link rel="icon" type="image/ico" href="/tools/dlpage/res/chrome/images/chrome-16.png"><title>Sheria na Masharti ya Google Chrome</title>
7 <style>
8 body { font-family:Arial; font-size:13px; }
9 </style>
10 <script type="text/javascript">
11 function carry_tracking(obj) {
12 var s = '(\\?.*)';
13 var regex = new RegExp(s);
14 var results = regex.exec(window.location.href);
15 if (results != null) {
16 obj.href = obj.href + results[1];
17 } else {
18 s2 = 'intl/([^/]*)';
19 regex2 = new RegExp(s2);
20 results2 = regex2.exec(window.location.href);
21 if (results2 != null) {
22 obj.href = obj.href + '?hl=' + results2[1];
26 </script></head>
28 <body>
29 <h2>Sheria na Masharti ya Google Chrome</h2>
30 <p>Sheria na Masharti haya yanatumika kwa toleo la hati fumbo la kutekelezwa la Google Chrome. Hati fumbo asili ya Google </p>
31 <p><strong>1. Uhusiano wako na Google </strong></p>
32 <p>1.1 Matumizi yako ya bidhaa, programu, huduma na tovuti za Google (kwa pamoja zikiitwa "Huduma" katika andiko hili na pasipo kujumuisha huduma zozote zinazotolewa kwako na Google chini ya mktaba tofauti ulioandikwa) yako chini ya masharti ya mkataba wa kisheria kati yako na Google. “Google” inamaanisha Google Inc., ambayo ofisi yake kuu iko 1600 Amphitheatre Parkway, Mountain View, CA 94043, Marekani. Andiko hili linaeleza jinsi mktaba ulivyo, na kuweka baadhi ya masharti ya mkataba huo.</p>
33 <p>1.2. Isipokuwa iwe imekubaliwa vingine kwa maandishi na Google, mkataba wako na Google utajumuisha kila wakati, kwa uchache, sheria na masharti yaliyowekwa katika andiko hili. Haya yanaitwa “Masharti ya Kijumla” hapa chini. Leseni za programu huria kwa hati fumbo asili za Google Chrome ni mikataba tofauti iliyoandikwa. Kadri leseni za programu huria zinavyochukua nafasi ya Masharti haya ya Kijumla, leseni za programu huria zinatawala mktaba wako na Google kwa matumizi ya Google Chrome au vipengee mahsusi vya Google Chrome vilivyojumuishwa.</p>
34 <p>1.3 Mkataba wako na Google pia utajumuisha masharti ya Arifa zozote za Kisheria zinazohusika na Huduma, pamoja na Masharti ya Kijumla. Haya yote yanaitwa “Masharti ya Ziada” hapa chini. Wakati Masharti ya Ziada yanatumika kwa Huduma, utaweza kuyapata na kuyasoma aidha ndani ya, au kupitia matumizi yako ya Huduma hiyo.</p>
35 <p>1.4 Masharti ya Kijumla, pamoja na Masharti ya Ziada, ni mkataba unaowajibisha kisheria kati yako na Google kuhusiana na matumizi yako ya Huduma. Ni muhimu kwako kuchukua wakati na kuyasoma kwa makini. Kwa pamoja, mkataba huu wa kisheria unaitwa “Masharti” hapo chini.</p>
36 <p>1.5 Ikiwa kuna mkinzano wowote kati ya Masharti ya Ziada na tuseme Masharti ya Jumla yanavyosema, basi Masharti ya Ziada yatachukua nafasi ya kwanza kuhusiana na Huduma hiyo.</p>
37 <p><strong>2. Kukubali Masharti</strong></p>
38 <p>2.1 Ili kutumia Huduma, sharti ukubali Masharti kwanza. Huwezi kutumia Huduma usipokubali Masharti.</p>
39 <p>2.2 Unaweza kukubali Masharti kwa:</p>
40 <p>(A) kubofya ili kukubali Masharti, wakati chaguo hili linatolewa kwano na Google katika kiolesura cha mtumiaji cha Huduma yoyote; au</p>
41 <p>(B) kwa kutumia Huduma zenyewe haswa. Katika hali hii, unaelewa na kukubali kuwa Google itachukulia matumizi yako ya Huduma kama kukubali kwa Masharti kuanzia hapo na kuendelea.</p>
42 <p><strong>3. Lugha ya Masharti </strong></p>
43 <p>3.1 Ambapo Google imekupatia tafsiri ya toleo la Kiingereza la Masharti, basi unakubali kuwa tafsiri hiyo imetolewa kwa manufaa yako tu na kuwa toleo la Masharti la lugha ya Kiingereza litasimamia uhusiana wako na Google.</p>
44 <p>3.2 Ikiwa kuna mkinzano wowote kati ya toleo la lugha ya Kiingereza la Masharti lisemavyo na tafsiri isemavyo, basi toleo la lugha ya Kiingereza litachukua nafasi ya kwanza.</p>
45 <p><strong>4. Utoaji Huduma wa Google</strong></p>
46 <p>4.1 Google ina biashara inazomiliki na huluki za kisheria inazoshirikishwa nazo ulimwenguni kote (“Kampuni Google inazomiliki na Washirika”). Wakati mwingine, kampuni hizi zitakuwa zikitoa Huduma kwako kwa niaba yake Google. Unatambua na kukubali kuwa Kampuni Google inazomiliki na Washirika wake watakuwa na haki ya kutoa Huduma kwako.</p>
47 <p>4.2 Google huwa inavumbua kila wakati ili kutoa hali nzuri iwezekanavyo kwa watumiaji wake. Unatambua na kukubali kuwa muundo na aina ya Huduma ambazo Google inatoa zinaweza kubadilika mara kwa mara bila yako kuarifiwa awali.</p>
48 <p>4.3 Kama sehemu ya uvumbuzi wake wa kila wakati, unatambua na kukubali kuwa Google inaweza kuacha (kabisa au kwa muda) kutoa Huduma (au vipengele vyovyote katika Huduma) kwako au kwa watumiaji kijumla kwa hiari ya Google peke yake, bila kutoa ilani yoyote kwako. Unaweza kuacha kutumia Huduma wakati wowote ule. Sio sharti uijulishe Google mahsusi unapoacha kutumia Huduma.</p>
49 <p>4.4 Unatambua na kukubali kuwa ikiwa Google italemaza mfiko wako kwa akaunti yako, unaweza kuzuiwa usipate huduma, maelezo ya akaunti yako au au faili zozote au maudhui menginyo yaliyo ndani ya akaunti yako.</p>
50 <p><strong>5. Matumizi yako ya Huduma</strong></p>
51 <p>5.1 Unakubali kutumia Huduma kwa madhumuni yanayokubaliwa na (a) Masharti na (b) na sheria au kanuni yoyote inayotumika au desturi inayokubalika pakubwa au miongozo katika eneo la utawala linalohusika (zikiwemo sheria zozote kuhusu uhamishaji wa data au programu kwenda na kutoka Marekani au nchi zingine husika).</p>
52 <p>5.2. Unakubali kuwa hautashiriki katika shughuli yoyote itakayoingilia au kukatiza Huduma (au seva na mitandao iliyounganishwa kwa Huduma).</p>
53 <p>5.3 Isipokuwa uwe umeruhusiwa mahsusi kufanya hivyo katika mkataba tofauti na Google, unakubali kuwa hautanakili, kurudufu, kuuza, kufanya biashara au kuuza tena Huduma kwa madhumuni yoyote.</p>
54 <p>5.4 Unakubali kuwa unawajibika peke yako kwa (na kuwa Google haina wajibu wowote kwako au mtu mwingine kwa) ukiukaji wowote wa wajibu wako chini ya Masharti na kwa matokeo (ikiwemo hasara yoyote au uharibifu ambao utaikumba Google) ya ukiukaji wowote kama huo.</p>
55 <p><strong>6. Faragha na maelezo yako ya kibinafsi</strong></p>
56 <p>6.1 Kwa maelezo kuhusu desturi za Google za ulinzi wa data, tafadhali soma sera ya faragha ya Google kwenye http://www.google.com/privacy.html. Sera hii inaeleza desturi za Google za ulinzi wa data, na kulinda faragha yako unapotumia Huduma.</p>
57 <p>Unakubali kutumia data yako kulingana na sera za faragha za Google.</p>
58 <p><strong>7. Maudhui katika Huduma</strong></p>
59 <p>7.1 Unaelewa kuwa maelezo yoyote (kama vile faili za data, maandishi, programu za kompyuta, faili za sauti au sauti zinginezo, picha, video na picha zinginezo) ambazo unaweza kuzifikia kama sehemu ya, au kupitia matumizi yako ya, Huduma ni jukumu la mtu ambaye maudhui kama hayo yalitoka. Maelezo yote kama hayo yanaitwa “Maudhui” hapa chini.</p>
60 <p>7.2 Unastahili kufahamu kuwa maudhui yanayowasilishwa kwako kama sehemu ya Huduma, yakiwemo lakini sio tu matangazo katika Huduma na Maudhui yaliyodhaminiwa katika Huduma huenda yakawa yamelindwa na haki za uvumbuzi zinazomilikiwa na wadhamini au watangazaji wanaotoa Maudhui hayo kwa Google (au kutoka kwa mtu mwingine au kampuni kwa niaba yao). Hauruhusiwi kubadilisha, kukodisha, kupangisha, kuuza, kusambaza au kuunda kazi kutokana na Maudhui haya (aidha sehemu yake au yote) isipokuwa uwe umeelezwa mahsusi kuwa unaweza kufanya hivyo na Google au wanaomiliki Maudhui hayo, katika mkataba tofauti.</p>
61 <p>7.3 Google inahifadhi haki (lakini haiwajibiki) kukagua kwanza, kutathmini, kualamisha, kuchuja, kubadilisha, kukataa au kuondoa Maudhui yoyote au yote kutoka kwenye Huduma yoyote. Kwa baadhi ya Huduma, Google inaweza kutoa zana za kuchuja na kuondoa maudhui waziwazi ya ngono. Zana hizi ni pamoja na mipangilio ya mapendeleo ya SafeSearch (tazama http://www.google.com/help/customize.html#safe). Zaidi ya hayo, kuna huduma na programu zinazouzwa za kuzuia mfiko kwa maudhui yanayokuchukiza.</p>
62 <p>7.4 Unaelewa kuwa kwa kutumia Huduma unaweza kupokea Maudhui unayoyadhania kuwa ya kuchukiza, machafu au yasiyostahimilika na kuwa, katika swala hili, unatumia Huduma kwa thubutu yako mwenyewe.</p>
63 <p>7.5 Unakubali kuwa unawajibika peke yako kwa (na kuwa Google haina wajibu wowote kwako au mtu mwingine kwa) Maudhui yoyote utakayounda, kuwasilisha au kuonyesha unapotumia Huduma na kwa matokeo ya vitendo vyako (ikiwemo hasara yoyote au uharibifu ambao utaikumba Google) kwa kufanya hivyo.</p>
64 <p><strong>8. Hakimilki mahsusi</strong></p>
65 <p>8.1. Unatambua na kukubali kuwa Google (au watoa leseni wa Google) inamiliki haki zote za kisheria, milki na maslahi katika na kwa Huduma, zikiwemo hakimilki zozote za uvumbuzi zinazodumu katika Huduma (iwe haki hizo zimesajiliwa au la, na popote ulimwenguni ambapo haki hizo zinadumu).</p>
66 <p>8.2 Isipokuwa umekubaliana vinginevyo na Google kwa maandishi, hakuna chochote katika Masharti haya kinachokupatia haki ya kutumia majina ya biashara, chapa-biashara, alama za huduma, nembo au majina ya vikoa vya Google, au vipengele vyovyote mahsusi vya chapa ya biashara. </p>
67 <p>8.3 Ikiwa umepewa haki mahsusi na Google ya kutumia yoyote ya vipengele hivi katika mkataba tofauti ulioandikwa, basi unakubali kuwa matumizi yako ya kila kipengee kama hicho yatakuwa kulingana na mkataba huo, kanuni zozote za Masharti zinazotumika na miongozo ya Google ya matumizi ya vipengele vya chapa ya biashara kama inavyosasishwa mara kwa mara. Unaweza kutazama mwongozo huu kwenye wavuti hapa http://www.google.com/permissions/guidelines.html (au URL nyingineyo itakayotolewa na Google kwa madhumuni haya mara kwa mara).</p>
68 <p>8.4 Google inatambua na kukubali kuwa haipati haki, milki au maslahi yoyote kutoka kwako (au watoa leseni wako) chini ya Masharti haya kwa Maudhui yoyote unayowasilisha, kuchapisha au kuonyesha kwenye, au kupitia Huduma, zikiwemo hakimilki zozote za uvumbuzi zinazodumu katika Maudhui hayo (iwe haki hizo zimesajiliwa au la, na popote ulimwenguni ambapo haki hizo zinadumu). Isipokuwa umekubaliana vingine na Google katika maandishi, unakubali kuwa unawajibika kulinda na kutekeleza haki hizo na kuwa Google haina wajibu wowote wa kufanya hivyo kwa niaba yako.</p>
69 <p>8.5 Unakubali kuwa hautaondoa, kuficha au kubadilisha ilani zozote za hakimilki mahsusi (zikiwemo ilani za hakimilki na chapa-biashara) ambazo zimeambatishwa au zilizo ndani ya Huduma.</p>
70 <p>8.6 Isipokuwa umepewa idhini mahsusi na Google kwa maandishi kufanya hivyo, unakubali kuwa katika kutumia Huduma, hautatumia chapa-biashara yoyote, alama za huduma, jina la biashara au nembo ya kampuni au shirika lolote kwa njia ambayo inaweza au inayonuiwa kuleta tashwishi kuhusu anayemiliki au mtumiaji aliyeidhinishwa wa alama, majina au nembo kama hizi.</p>
71 <p><strong>9. Leseni kutoka Google </strong></p>
72 <p>9.1 Google inakupatia leseni ya kibinafsi, ulimwenguni kote, bila malipo, isiyoweza kuhamiswa na isiyo mahsusi kutumia programu iliyotolewa kwako na Google kama sehemu ya Huduma inavyotolewa kwako na Google (inaitwa “Programu” hapa chini). Leseni hii na kwa madhumuni tu ya kukuwezesha kutumia na kufurahia manufaa ya Huduma jinsi zinavyotolewa na Google, katika njia iliyokubaliwa katika Masharti.</p>
73 <p>9.2 Kulingana na sehemu ya 1.2, huruhusiwi (na hupaswi kumruhusu mtu yeyote) kunakili, kubadilisha, kuunda kazi kutokana na, kufanya uhandisi kwa kupambua, kupambua au kwa vinginevyo kujaribu kudondoa hati fumbo asili ya programu au sehemu yoyote yake, isipokuwa hii imeruhusiwa kimahsusi au kuhitajika kisheria, au isipokuwa Google imekwambia kimahsusi kuwa waweza kufanya hivyo kwa maandishi.</p>
74 <p>9.3 Kulingana na sehemu ya 1.2, isipokuwa Google imekupatia ruhusa mahsusi kwa maandishi kufanya hivyo, hauruhusiwi kutoa (au kutoa leseni ndogo ya) haki zako za kutumia Programu, kutoa maslahi ya usalama katika au juu ya haki zako za kutumia Programu, au kwa vinginevyo kusihia sehemu yoyote ya haki zako za kutumia Programu.</p>
75 <p><strong>10. Leseni ya maudhui kutoka kwako</strong></p>
76 <p>10.1 Unahifadhi hakimilki na haki zingine zozote ambazo tayari unazo kwa Maudhui unayowasilisha, kuchapisha au kuonyesha kwenye au kupitia, Huduma.</p>
77 <p><strong>11. Sasisho za programu</strong></p>
78 <p>11.1 Programu unayotumia inaweza kupakua na kusakinisha sasisho kutoka Google kiatomatiki mara kwa mara. Sasisho hizi zimeundwa ili kuboresha, kukoleza na kuendeleza Huduma na zinaweza kuwa marekebisho ya hitilafu, uboreshaji wa utendaji, sehemu mpya za programu na matoleo mapya kabisa. Unakubali kupokea sasisho kama hizo (na unaruhusu Google kuziwasilisha kwako) kama sehemu ya matumizi yako ya Huduma.</p>
79 <p><strong>12. Kumaliza uhusiano wako na Google</strong></p>
80 <p>12.1 Masharti haya yataendelea kutumika hadi yatanguliwe aidha nawe au na Google kama ilivyoelezwa hapa chini.</p>
81 <p>12.2 Google inaweza, wakati wowote, kutangua mkataba wake wa kisheria nawe ikiwa:</p>
82 <p>(A) umekiuka kanuni yoyote ya Masharti (au umefanya mambo kwa njia inayoonyesha waziwazi kuwa haunuii, au hauwezi kutii kanuni za Masharti); au</p>
83 <p>(B) Google inahitajika kufanya hivyo na sheria (kwa mfano, ambapo kutoa Huduma kwano ni, au kumekuwa, sio halali kisheria); au</p>
84 <p>(C) mshirika ambaye Google alitoa huduma kwako naye ameumaliza uhusiano wake na Google au ameacha kutoa Huduma kwako; au</p>
85 <p>(D) Google inaelekea kuacha kutoa Huduma kwa watumiaji katika nchi unamoishi au unayotumia Huduma kutoka kwake; au</p>
86 <p>(E) Google kutoa Huduma kwako, kwa maoni ya Google, hakuna faida ya kibiashara tena.</p>
87 <p>12.3 Hakuna chochote katika Sehemu hii kitakachoathiri haki za Google kuhusiana na utoaji wa Huduma chini ya Sehemu ya 4 ya Masharti haya.</p>
88 <p>12.4 Masharti haya yatakapokoma, na haki, wajibu na dhima zote za kisheria ambazo wewe na Google mmenufaika nazo, mmetii (au ambazo zimepatikana kwa muda ambao Masharti yametumika) au ambayo yamesemwa kuwa yataendelea bila kikomo, hayataathiriwa na kukoma huku, na kanuni za aya ya 19.7 zitaendelea kutekeleza haki, wajibu na dhima kam hizo bila kikomo.</p>
89 <p><strong>13. KUONDOLEWA KWA ARABUNI</strong></p>
90 <p>13.1 HAKUNA CHOCHOTE KATIKA MASHARTI HAYA, ZIKIWEMO SEHEMU ZA 13 NA 14, KITAKACHOONDOA AU KUWEKA MPAKA ARABUNI AU DHIMA YA GOOGLE KWA HASARA AMBAZO HUENDA HAZIJAONDOLEWA AU KUWEKWA MIPAKA NA SHERIA ZINAZOTUMIKA. MAENEO FULANI YA UTAWALA HAYARUHUSU KUONDOLEWA KWA ARABUNI AU MASHARTI FULANI AU KUONDOLEWA KWA DHIMA KWA HASARA AU UHARIBIFU UNAOSABABISHWA NA ULEGEVU, UKIUKAJI WA MKATABA AU UKIUKAJI WA MASHARTI YASIYOTAJWA AU FIDIA ZINAZOHUSIANA AU ZINAZOAMBATANA. KAMA IPASAVYO, MIPAKA ILIYO HALALI KISHERIA KATIKA ENEO LAKO LA UTAWALA ITATUMIKA KWAKO NA DHIMA YETU ITAKUWA NA KIKOMO KADRI INAYVYOKUBALIWA NA SHERIA.</p>
91 <p>13.2 UNAELEWA NA KUKUBALI KIMAHSUSI KUWA MATUMIZI YAKO YA HUDUMA NI KWA THUBUTU YAKO MWENYEWE TU NA KUWA HUDUMA ZINATOLEWA &quot;JINSI ZILIVYO&quot; NA “KAMA ZINAVYOPATIKANA.”</p>
92 <p>13.3 HUSUSAN, GOOGLE, KAMPUNI INAZOMILIKI NA WASHIRIKA WAKE NA WATOA LESENI WAKE HAWAWAKILISHI AU KUKUHAKIKISHIA KUWA:</p>
93 <p>(A) MATUMIZI YAKO YA HUDUMA YATATIMIZA MAHITAJI YAKO,</p>
94 <p>(B) MATUMIZI YAKO YA HUDUMA HAYATAKATIZWA, YATAPATIKANA KWA MUDA UFAAO, YATAKUWA SALAMA NA BILA HITILAFU,</p>
95 <p>(C) MAELEZO YOYOTE UNAYOYAPATA KUTOKANA NA MATUMIZI YAKO YA HUDUMA YATAKUWA SAHIHI AU YA KUTEGEMEKA, NA</p>
96 <p>(D) KUWA UPUNGUFU WOWOTE KATIKA UENDESHAJI AU UTENDAJI WA PROGRAMU INAYOTOLEWA KWAKO KAMA SEHEMU YA HUDUMA ITAREKEBISHWA.</p>
97 <p>13.4 KITU CHOCHOTE KILICHOPAKULIWA AU KUPATIKANA VINGINE KUPITIA MATUMIZI YA HUDUMA NI KWA HIARI NA THUBUTU YAKO MWENYEWE NA KUWA UTAWAJIBIKA PEKE YAKO KWA HASARA YOYOTE KWA MFUMO WAKO WA KOMPYUTA AU KIFAA KINGINECHO AU KUPOTEZA DATA KUTOKANA NA KUPAKUA KITU CHOCHOTE KAMA HICHO.</p>
98 <p>13.5 HAKUNA MAWAIDHA WALA MAELEZO, YALIYOTAMKWA AU KUANDIKWA, YATAKAYOPATIKANA NAWE KUTOKA KWA GOOGLE AU KUPITIA HUDUMA YATAUNDA ARABUNI YOYOTE ISIYOTAJWA KIMAHSUSI KATIKA MASHARTI.</p>
99 <p>13.6 GOOGLE VILEVILE INAKANUSHA KIMAHSUSI ARABUNI NA MASHARTI YA AINA YOYOTE, YAWE MAHSUSI AU YASIYOTAJWA, PAMOJA NA, NA SIO TU ARABUNI ZISIZOTAJWA NA MASHARTI YA KUFAA KWA MAUZO, KUFAA KWA MADHUMUNI FULANI NA DHIDI YA UKIUKAJI.</p>
100 <p><strong>14. KIKOMO CHA DHIMA</strong></p>
101 <p>14.1 KULINGANA NA KANUNI KATIKA AYA YA 13.1 HAPO JUU, UNAELEWA KIMAHSUSI NA KUKUBALI KUWA GOOGLE, KAMPUNI INAZOMILIKI NA WASHIRIKA WAKE, NA WATOA LESENI WAKE HAWATAKUWA NA DHIMA KWAKO KWA:</p>
102 <p>(A) HASARA YOYOTE ILIYO NA ISIYO YA MOJA KWA MOJA, YA KUAMBATANA, MAHSUSI, AU YA ADHABU INAYOWEZA KUKUPATA, IWE IMESABABISHWA VIPI AU CHINI YA KANUNI YOYOTE YA DHIMA. HII ITAJUMUISHA, LAKINI SIO TU, KUPOTEZA FAIDA YOYOTE (IWE IMETOKEA KWA NJIA YA MOJA KWA MOJA AU LA), KUPOTEZA UFADHILI AU SIFA YOYOTE YA BIASHARA, KUPOTEZA DATA YOYOTE, GHARAMA YA KUNUNUA BIDHAA AU HUDUMA MBADALA, AU HASARA NYINGINEYO ISIYO DHAHIRI;</p>
103 <p>(B) HASARA AU UHARIBIFU UNAOWEZA KUKUPATA, IKIWEMO NA SIO TU HASARA AU UHARIBIFU KUTOKANA NA:</p>
104 <p>(I) KUTEGEMEA KWAKO UKAMILIFU, USAHIHI AU UWEPO WA MATANGAZO YOYOTE, AU KUTOKANA NA UHUSIANO WOWOTE AU BIASHARA YOYOTE KATI YAKO NA MTANGAZAJI AU MDHAMINI YEYOTE AMBAYE MATANGAZO YAKE HUTOKEA KWENYE HUDUMA;</p>
105 <p>(II) MABADILIKO YOYOTE AMBAYO GOOGLE INAWEZA KUFANYA KWA HUDUMA, AU KUSITISHWA KWA MUDA AU KABISA KWA UTOAJI WA HUDUMA (AU VIPENGEE VYOVYOTE KATIKA HUDUMA);</p>
106 <p>(III) KUFUTWA, KUHARIBIWA AU KUSHINDWA KUHIFADHIWA, KWA MAUDHUI YOYOTE AU DATA YOYOTE YA MAWASILIANO INAYODUMISHWA AU KUWASILISHWA NA AU KUPITIA MATUMIZI YAKO YA HUDUMA;</p>
107 <p>(IV) KUSHINDWA KWAKO KUTOA MAELEZO SAHIHI YA AKAUNTI KWA GOOGLE;</p>
108 <p>(V) KUSHINDWA KWAKO KUHIFADHI MAELEZO YA NENOSIRI LAKO NA AKAUNTI YAKO KWA USALAMA NA SIRI;</p>
109 <p>14.2 MIPAKA YA DHIMA YA GOOGLE KWAKO KATIKA AYA YA 14.1 HAPO JUU ITATUMIKA IKIWA GOOGLE IMEJULISHWA AU INGESTAHILI KUFAHAMU UWEZEKANO WA HASARA KAMA HIZO KUTOKEA AU LA.</p>
110 <p><strong>15. Sera za hakimilki na chapa biashara</strong></p>
111 <p>15.1 Ni sera ya Google kujibu arifa za ukiukaji wa hakimilki zinazotii sheria za hakimilki za kimataifa zinazohusika (ikiwemo, Marekani, Sheria ya Millennia ya Hakimilki Tarakinishi) na kufunga akaunti za wanaorudia ukiukaji. Maelezo ya sera ya Google yanaweza kupatikana kwenye http://www.google.com/dmca.html.</p>
112 <p>15.2 Google hutumia utaratibu wa malalamishi kuhusu chapa-biashara kuhusiana na shughuli za utangazaji za Google, maelezo yake ambayo yanapatikana http://www.google.com/tm_complaint.html.</p>
113 <p><strong>16. Matangazo</strong></p>
114 <p>16.1 Baadhi ya Huduma zinadhaminiwa na mapato kutoka kwa matanagazo na zinaweza kuonyesha matangazo na kampeni za matangazo. Matangazo hayo yanaweza kuwa yanalenga maudhui ya maelezo yaliyohifadhiwa kwenye Huduma, hoja zilizoulizwa kupitia Huduma au maelezo mengineyo.</p>
115 <p>16.2 Mbinu, hali na kiwango cha matangazo kutoka kwa Google kwenye Huduma kinaweza kubadilika bila ilani mahsusi kwako.</p>
116 <p>16.3 Kwa sababu Google inakuruhusu kupata na kutumia Huduma, unakubali kuwa Google inaweza kuweka matangazo kama hayo kwenye Huduma.</p>
117 <p><strong>17. Maudhui mengineyo</strong></p>
118 <p>17.1 Huduma zinaweza kujumuisha viungo kwa tovuti zingine, maudhui au nyenzo zingine. Google huenda isiwe na udhibiti wowote juu ya tovuti zozote au nyenzo zinazotolewa na watu au kampuni tofauti na Google.</p>
119 <p>17.2 Unatambua na kukubali kuwa Google haiwajibiki kwa upatikanaji wa tovuti zozote au raslimali kama hizo za nje, na haiidhinishi matangazo, bidhaa au vitu vyovyote kwenye au vinavyopatikana kwenye tovuti au nyenzo hizo.</p>
120 <p>17.3 Unatambua na kukubali kuwa Google haiwajibiki kwa hasara au uharibifu wowote unaoweza kukupata wewe kwa sababau ya upatikanaji wa tovuti au raslimali hizo za nje, au kutokana nawe kutegemea kwa vyovyote ukamilifu, usahihi au uwepo wa matangazo, bidhaa au vitu vyoyvote kwenye, au kutoka kwa, tovuti au nyenzo kama hizo.</p>
121 <p><strong>18. Mabadiliko kwa Masharti</strong></p>
122 <p>18.1 Google inaweza kufanya mabadiliko kwa Masharti ya Kijumla au Masharti ya Ziada mara kwa mara. Mabadiliko hayo yanapofanywa, Google itatoa nakala mpya ya Masharti ya Kijumla kwenye http://accounts.google.com/TOS?hl=en na Masharti yoyote mapya ya Ziada yatatolewa kwako kutoka ndani, au kupitia, Huduma zilizoathirika.</p>
123 <p>18.2 Unaelewa na kukubali kuwa ikiwa utatumia Huduma baada ya tarehe Masharti ya Kijumla au Masharti ya Kijumla kubadilika, Google itachukulia matumizi yako kuwa kukubali kwa Sheria na Mashati au Masharti ya Ziada yaliyosasishwa.</p>
124 <p><strong>19. Masharti ya kijumla ya kisheria</strong></p>
125 <p>19.1 Wakati mwingine ukitumia Huduma, unaweza (kwa sababu ya, au kuhusiana na matumizi yako ya Huduma) kutumia huduma au kupakua programu, au kununua bidhaa, zinazotolewa na mtu au kampuni nyingine. Matumizi yako ya huduma, programu au bidhaa hizi zingine zinaweza kuwa chini ya masharti tofauti katika yako na kampuni au mtu anayehusika. Ikiwa ni hivyo, Masharti haya hayaathiri uhusiano wako wa kisheria na kampuni hizo au watu hao wengine.</p>
126 <p>19.2 Masharti haya yanajumuisha mkataba wote wa kisheria kati yako na Google na yanatawala matumizi yako ya Huduma (lakini haijumishi huduma zozote ambazo Google inatoa kwako chini ya mkata tofauti ulioandikwa), na inachukua kabisa nafasi ya mikataba yoyote ya awali kati yako na Google kuhusiana na Huduma.</p>
127 <p>19.3 Unakubali kuwa Google inaweza kukupatia ilani, pamoja na zile zinazohusu mabadiliko kwa Masharti, kwa barua pepe au machapisho kwenye Huduma.</p>
128 <p>19.4 Unakubali kuwa ikiwa Google haitatumia au kutekeleza haki yoyote au suluhu ya kisheria iliyo katika Masharti (au ambayo Google inafaidika nayo chini ya sheria yoyote inayotumika), hii haitachukuliwa kuwa Google imesalimu kirasmi haki zake na kuwa Google bado itaweza kupata haki na suluhu hizo.</p>
129 <p>19.5 Ikiwa mahakama yoyote ya sheria, iliyo na mamlaka ya kuamua kuhusu swala hili, itaamua kuwa kanuni yoyote ya Masharti haya sio halali, basi kanuni hiyo itaondolewa kwenye Masharti bila kuathiri Masharti yaliyosalia. Kanuni za Masharti zilizosalia zitaendelea kuwa halali na kutumika.</p>
130 <p>19.6 Unatambua na kukubali kuwa kila mshirika wa kundi la kampuni ambalo Google ndio mmiliki atakuwa mfaidi wa nje wa Masharti haya na kuwa kampuni zingine kama hizo zitakuwa na haki ya kutekeleza moja kwa moja, na kutegemea, kanuni zozote za Masharti zinazokidhi manufaa juu (au haki kwa faida) yao. Isipokuwa hawa, hakuna mtu au kampuni nyinginee itakayokuwa mfaidi wa nje wa Masharti haya.</p>
131 <p>19.7 Masharti, na uhusiano wako na Google chini ya Masharti hayo, yatasimamiwa na sheria za Jimbo la California bila kuzingatia kanuni zake kwa sheria pinzani. Wewe na Google mnakubali kutii mamlaka ya mahakama zilizo katika wilaya ya Santa Clara, California peke yake kutatua swala lolote la kisheria litakalotokea kutokana na Masharti haya. Licha ya hayo, unakubali kuwa Google bado itaruhusiwa kufanya maombi ya suluhu za vizuizi (au aina sawa ya suluhu la dharura la kisheria)</p>
132 <p><strong>20. Masharti ya Ziada kwa Viendelezi vya Google Chrome</strong></p>
133 <p>20.1 Masharti katika sehemu hii yanatumika ukisakinisha viendelezi kwenye nakala yako ya Google Chrome. Viendelezi ni programu ndogo, zilizoundwa na Google au watu wengine, zinazoweza kubadilisha au kuboresha utendaji wa Google Chrome. Viendelezi vinaweza kuwa mfiko zaidi kwa kivinjari chako au kompyuta yako kuliko kurasa za wavuti za kawaida, ukiwemo uwezo wa kusoma na kubadilisha sehemu ya data yako ya kibinafsi.</p>
134 <p>20.2 Mara kwa mara, Google Chrome inaweza kuchunguza seva za mbali (zilizopangishwa na Google au wengine) kupata sasisho kwa viendelezi, yakiwemo lakini sio tu marekebisho ya hitilafu au kuboresha utendaji. Unakubali kuwa sasisho kama hizo zitaitishwa, kupakuliwa na kusakinishwa bila ya kukuarifu tena.</p>
135 <p>20.3 Mara kwa mara, Google inaweza kugundua kiendelezi kinachokiuka masharti ya Google kwa wasanidi programu au mikataba ya kisheria, sheria, kanuni au sera zingine. Google Chrome itapakua orodha ya viendelezi kama hivyo kutoka kwenye seva za Google. Unakubali kuwa Google inaweza kulemaza au kuondoa kwa mbali viendelezi kama hivyo kutoka kwenye mifumo ya watumizi kwa hiari yake pekee. </p>
136 <p>Tarehe 20 Oktoba, 2009</p>
137 </body>
138 </html>